Mapema Agosti 2019, Bodi inayoshughulikia Ujenzi na Maendeleo ya LAPSSET (LCDA) ilitangaza kukamilika kwa kiegesho hicho cha kwanza huku viegesho vingine viwili vya kwanza vikitarajiwa kukamilika kufikia Desemba 2020.
Afisa Mkuu Mtendaji wa LAPSSET, Bw Silvestre Kasuku, amesema kwamba wameshuhudia kampuni nyingi za meli ambazo hivi karibuni zimekuwa zikizuru bandari ya Lamu ili kutafuta mwanya na fursa za kibiashara na uwekezaji pindi LAPSSET itakapoanza kutekeleza shughuli zake rasmi.
Inatarajiwa kwamba baadaye Oktoba, kiegesho hicho cha kwanza kitafunguliwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Miongoni mwa kampuni tajika za usafiri wa meli ulimwenguni ambazo zimezuru bandari ya Lamu ni pamoja na Maersk kutoka Denmark, Evergreen Marine Corp, Mediterranean Shipping Company (MSC), Pacific International Line (PIL), Ocean Network Express (ONE), Hapag Lloyd, CMA CGM Group, China Ocean Shipping (Group) Company-COSCO na Hyundai Merchant Marine (HMM).
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |