• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • URA yafunga biashara kadhaa

    (GMT+08:00) 2019-10-18 17:16:59
    Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Uganda, URA yamefunga baadhi ya biashara katika mkoa wa Soroti, baada ya wamiliki wake kukwepa kulipa ushuru wa mamilioni ya pesa. Maduka makuu, hoteli za Kifahari na biashara zingine ndogo ndogo zilifungwa.

    Baadaye, maafisa wa usalama wa serikali walichukuwa usukani wa kulinda maeneo hayo hadi pale wamiliki wake watakapo lipa ushuru kwa serikali. Kwa sasa wafanyibiashara walioathirika na hatua hii ya URA, wameanza harakati ya kulipa malimbikizi yao ya ushuru kwa serikali.

    URA imetoa shinikizo kwa wamiliki wa biashara mbali mbali kuwajibika na kulipa ushuru kwa wakati ufaao ili kuepuka kufungiwa biashara zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako