• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wauza vyuma chakavu wafutiliwa leseni zao

    (GMT+08:00) 2019-10-18 17:17:16
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene, ameagiza kufutwa kwa vibali vya wafanyabiashara wote wanaosafirsha vyuma chakavu ambao hawakufuata maelekezo na maagizo ya Serikali.

    Amesema hayo jijini Dodoma wakati wa mkutano wa kupokea ripoti ya kamati aliyoiunda kwa ajili ya uchunguzi wa makontena ya bidhaa za chuma chakavu yaliyokuwa yamekamatwa kwa uchunguzi katika bandari ya jiji la Dar es Salaam.

    Aliongeza kuwa Wafanyabiashara wa vyuma chakavu siyo wakweli kwa sababu wengi wanasafirisha bidhaa zingine tofauti na vyuma chakavu huku wakisingizia kuwa wamebeba vyuma chakavu wakati siyo kweli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako