• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China apongeza kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa mtandao wa kiviwanda

    (GMT+08:00) 2019-10-18 19:06:16

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa mkutano wa kimataifa wa mtandao wa kiviwanda uliofanyika leo mjini Shenyang, kaskazini mashariki mwa China.

    Kwenye salamu hiyo, rais Xi amesema, kuendana na mageuzi mapya ya sayansi na teknolojia na mabadiliko ya mfumo wa kiviwanda, teknolojia ya mtandao wa kiviwanda imepiga hatua kubwa itakayotoa nguvu kwa uvumbuzi wa uchumi wa nchi mbalimbali na kutoa fursa mpya kwa maendeleo ya pamoja ya viwanda vya dunia.

    Rais Xi pia amesema, China inazingatia sana maendeleo ya mtandao wa kiviwanda, na inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuongeza uwezo wa uvumbuzi wa mtandao wa kiviwanda ili kutimiza maendeleo ya kina zaidi ya viwanda na teknolojia ya habari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako