• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kuona nchi za Afrika zinanufaika zaidi na maendeleo yake

    (GMT+08:00) 2019-10-18 19:23:10

    China inapenda kuimarisha ushirikiano na Afrika katika sekta za viwanda, miundombinu, pamoja na biashara na uwekezaji, ili nchi za Afrika zinufaike zaidi na maendeleo yake na watu wa pande hizo mbili wapate manufaa halisi.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema hayo leo hapa Beijing baada ya awamu ya kwanza ya mradi uliofanywa na kampuni la China wa reli ya kisasa ya kutoka Nairobi hadi Malaba, nchini Kenya kuzinduliwa tarehe 16, na China na Mauritius kusaini makubaliano ya biashara huria tarehe 17. Bw. Geng amesema hivi sasa China na nchi za Afrika zinatekeleza ipasavyo matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Beijing na kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Anasema, "Uzinduzi wa awamu ya kwanza ya reli ya Nairobi-Malaba na utiaji saini wa makubaliano ya biashara huria kati ya China na Mauritius ni matokeo mapya ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuonyesha nia imara na maendeleo mazuri ya ushirikiano wa kunufaishana wa kutafuta maendeleo ya pamoja kati ya pande hizo mbili. China ikiwa mwenzi, rafiki na ndugu wa nchi za Afrika, siku zote inaangalia mahitaji ya nchi za Afrika, kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Afrika, kushiriki kwenye ujenzi wa miundombinu barani humo na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako