• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii katika mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-10-18 19:54:17

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang leo hapa Beijing amesema, ingawa uchumi wa China unakabiliwa na changamoto inayotokana na hali ya dunia, lakini umedumisha maendeleo ya utulivu katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu, na China itatimiza malengo yake ya mwaka huu ya maendeleo ya uchumi na jamii.

    Bw. Li ameyasema hayo alipokutana na wajumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Ushauri wa Sekta ya Uzalishaji wa Hali ya Juu. Amesema serikali ya China imetoa mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya uchumi kupitia hatua chanya za kupunguza ushuru, kuondoa vikwazo vya kuingia sokoni, kufanya usimamizi wenye usawa na haki, na kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za kiubunifu. Ameongeza kuwa China inakaribisha makampuni ya kimataifa kushirikiana nayo kupanua soko, ili kupata mafanikio kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako