• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michezo ya 7 ya majeshi duniani yafunguliwa

    (GMT+08:00) 2019-10-19 18:26:08

    Michezo ya 7 ya majeshi duniani ilifunguliwa jana huko Wuhan, mji wa katikati nchini China. Rais Xi Jinping wa China alihudhuria sherehe ya ufunguzi na kutangaza kufunguliwa kwa michezo hiyo.

    Hii ni mara ya kwanza kwa michezo hiyo kufanyika nchini China, na itafanyika kwa siku kumi kwa kauli mbiu ya "marafiki na kujenga amani kwa pamoja". Karibu wanajeshi elfu kumi kutoka nchi zaidi ya 100 wamejiandikisha kushiriki kwenye michezo hiyo. Kwa ujumla kuna shughuli kubwa za michezo 27 na shughuli ndogo za michezo 329, kama vile kulenga shabaha, kuogelea, riadha na mpira wa kikapu. Hii ndio idadi kubwa kabisa ya shughuli za michezo katika historia ya michezo ya majeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako