• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yahimiza pande zote kusuluhisha mvutano wa kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-10-20 18:17:00

    Kamati ya fedha na mambo ya fedha, ambayo ni chombo cha kutoa maamuzi katika Shirika la fedha duniani (IMF)imehimiza pande zote kusuluhisha mvutano wa kibiashara na kuunga mkono mageuzi ya lazima ya Shirika la biashara duniani (WTO) ili kukuza ukuaji wa uchumi wa dunia.

    Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa 40 wa mawaziri wa kamati hiyo kumalizika inasema kuwa kutokana na uwepo kwa mvutano wa kibiashara, sera zisizo na uhakika, hatari za siasa za kikanda, uchumi wa dunia unatazamiwa kuzidi kudidimia.

    Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni gavana wa Benki kuu ya Afrika Kusini Lesetja Kganyago alisisitiza kuwa, biashara ya kimataifa ni uti wa mgongo wa uchumi wa dunia, kwa hiyo katika vita vya biashara hakuna mshindi, ila tu uchumi wa dunia utapata hasara kubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako