• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti mpya yasema idadi ya watumiaji wa mtandao wa kasi nchini China inaongoza duniani

    (GMT+08:00) 2019-10-21 08:57:26

    Ripoti mpya kuhusu Maendeleo ya Mtandao wa Internet Nchini China imetolewa rasmi kwenye Mkutano wa sita wa Internet Duniani unaofanyika huko Wuzhen, mkoani Zhejiang, China.

    Ripoti hiyo imesema zaidi ya asilimia 90 ya watumiaji wa huduma za Internet nchini China wanajiunga na mtandao kupitia mkonga wa mawasiliano 'Fibre Optic', idadi inayochukua nafasi ya kwanza duniani. Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, idadi ya watumiaji wa mtandao kupitia mkonga wa mawasiliano 'Fibre Optic' nchini China imefikia milioni 396, ikichukua asilimia 91 ya watumiaji wote wa mtandao wa kasi nchini.

    Ripoti inaona kuwa kutokana na China kuendelea kusukuma mbele ujenzi wa miundombinu ya Tehama, uwezo wa mtandao nchini humo umeinuka kidhahiri. Baada ya serikali kutoa leseni za matumizi ya kibiashara ya teknolojia ya 5G mwezi Juni mwaka huu, China imeingia rasmi kwenye zama ya 5G.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako