• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la tisa la Xiangshan la Beijing lafunguliwa

    (GMT+08:00) 2019-10-21 17:05:26

    Kongamano la tisa la Xiangshan la Beijing limefunguliwa leo katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Beijing. Waziri wa ulinzi wa China Bw. Wei Fenghe amehudhuria ufunguzi wa mkutano huo, na kusoma barua ya pongezi kutoka kwa rais Xi Jinping wa China.

    Kwenye barua hiyo, rais Xi amesema China inashikilia kuhimiza ushirikiano kupitia mazungumzo, kuhimiza amani kupitia ushirikiano, na kuhakikisha maendeleo kupitia amani, kwani amani ni tumaini la watu wote duniani. Amesisitiza kuwa kulinda amani na utulivu wa kudumu katika kanda ya Asia na Pasifiki kunaendana na maslahi ya pamoja ya nchi za kanda hiyo. Nchi zote husika zinapaswa kushikamana na kulinda kithabiti mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kuendelea kuboresha uhusiano mpya wa wenzi wa usalama, na kuhimiza kujenga mfumo wa usalama unaolingana na hali halisi ya maendeleo ya kikanda, ili kuhimiza amani ya kudumu na usalama katika kanda ya Asia na Pasifiki. Pia kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza maendeleo ya amani ya dunia na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Bw. Wei Fenghe amesema, katika zama mpya, siku zote jeshi la China linafuata njia ya kujiendeleza kwa amani, na kushikilia sera ya ulinzi ya kujilinda. Kwa sasa, mfumo na utaratibu wa usalama wa kimataifa unakabiliwa na changamoto kubwa, hivyo kushikilia kuheshimiana na kutimiza kunufaiashana ni matumaini ya pamoja ya nchi zote duniani. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi husika katika kuhimiza ujenzi wa kanuni ya usalama katika kanda ya Asia na Pasifiki, kuboresha mfumo wa pande nyingi wa usalama, kuanzisha uhusiano mpya wa wenzi wa usalama, na kufanya ushirikiano wa kijeshi kwa ajili ya usalama wa kanda ya Asia na Pasifiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako