• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za uchukuzi wa meli zafurika Lamu kutafuta fursa za kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-10-21 21:08:56

    KAMPUNI 10 za usafiri wa meli zinazoongoza ulimwenguni ni miongoni mwa 40 ambazo tayari zimezuru Bandari Mpya ya Lamu (LAPSSET) wakati ambapo kiegesho cha kwanza cha mizigo bandarini humo kinatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi huu wa Oktoba.

    Mapema Agosti 2019, Bodi inayoshughulikia Ujenzi na Maendeleo ya LAPSSET (LCDA) imetangaza kukamilika kwa kiegesho hicho cha kwanza huku viegesho vingine viwili vya kwanza vikitarajiwa kukamilika kufikia Desemba 2020.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa LAPSSET, Bw Silvestre Kasuku, amesema wameshuhudia kampuni nyingi za meli ambazo hivi karibuni zimekuwa zikizuru bandari ya Lamu ili kutafuta mwanya na fursa za kibiashara na uwekezaji pindi LAPSSET itakapoanza kutekeleza shughuli zake rasmi.

    Bandari ya Lamu itahudumia soko la nchi ya Ethiopia ambayo kwa sasa hutegemea bandari ya Djibouti na ile ya Sudan Kusini katika shughuli zake za uchukuzi wa mizigo.

    Bandari ya Lamu inajumuisha viegesho 32 wakati itakapokuwa imekamilika.

    Miongoni mwa kampuni tajika za usafiri wa meli ulimwenguni ambazo zimezuru bandari ya Lamu ni pamoja na Maersk kutoka Denmark, Evergreen Marine Corp, Mediterranean Shipping Company (MSC), Pacific International Line (PIL), Ocean Network Express (ONE), Hapag Lloyd, CMA CGM Group, China Ocean Shipping (Group) Company-COSCO na Hyundai Merchant Marine (HMM).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako