• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 14 wauawa katika shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la Afghanistan

    (GMT+08:00) 2019-10-22 16:55:28

    Taarifa iliyotolewa na jeshi la Afghanistan imesema wapiganaji 14 wa kundi la Taliban wamethibitishwa kuuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi la anga lililofanywa na ndege za jeshi la Afghanistan dhidi ya maficho ya wapiganaji wa kundi hilo katika wilaya ya Darqad, mkoa wa Takhar, kaskazini mwa nchi hiyo.

    Kundi la Taliban halijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.

    Katika miaka ya karibuni, mkoa wa Takhar umeshuhudia ongezeko la mashambulizi yanayofanywa na kundi la Taliban.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako