Naibu mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Hazina katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bw. Paolo Mauro ameipongeza China kwa kuchukua nafasi yake katika vitendo vya pamoja vya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua kando ya mkutano wa mwaka wa IMF na Benki ya Dunia uliofanyika mjini Washington, Marekani, Bw. Mauro amesema China ni nchi muhimu, sio tu kwa uchumi wa dunia, bali pia katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema China inachukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya jewa na imepata mafanikio dhahiri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |