• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaheshimu na kulinda kikamilifu uhuru wa kujieleza wa raia

    (GMT+08:00) 2019-10-22 17:20:23

    Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umefanya majadiliano maalum juu ya suala la uhuru wa kujieleza.

    Akizungumzia mkutano huo, mjumbe maalumu wa Wizara ya mambo ya nje ya China anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu Bibi Liu Hua amesema, Katiba na sheria nyingine za China zinaheshimu na kulinda kikamilifu uhuru wa kujieleza wa raia. Serikali ya China inafanya juhudi za kuwapatia raia nafasi nyingi zaidi za kujieleza, kuzingatia maoni ya raia katika kufanya uvumbuzi wa kuboresha njia za usimamizi, na kuweka jukwaa la kujieleza kupitia mtandao wa internet.

    Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuheshimu haki ya uhuru wa kujieleza wa raia, pia inatakiwa kujenga utaratibu wa utawala wa sheria kwa mujibu wa sheria. Nchi zote zinatakiwa kufanya mazungumzo na ushirikiano chini ya msingi wa kuheshimiana na kuweka kanuni ya utawala wa mtandao wa Internet inayotumika dunia nzima.

    Wakati huohuo, Bibi Liu Hua amezungumzia suala la haki za walemavu na kusema, serikali ya China inatilia maanani sana na kuhimiza kulinda haki zote za walemavu. Katika mchakato wa ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote utakaomalizika mwakani, mlemavu yeyote wa China hataachwa nyuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako