• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapanga kurekebisha sheria mbili kuhusu ulinzi wa haki za watoto wadogo

    (GMT+08:00) 2019-10-22 17:40:23

    Kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China imeanza mchakato wa kukagua na kuthibitisha mswada wa marekebisho ya Sheria ya kulinda watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 na mswada wa marekebisho ya sheria ya kuzuia uhalifu wa watoto wadogo, sheria ambazo zilitungwa katika miaka ya 90 ya karne iliyopita. Hii ni mara ya kwanza kufanya marekebisho makubwa juu ya sheria hizo mbili tangu zilipoanza kutekelezwa baada ya kurekebishwa miaka 7 iliyopita. Miswada hiyo miwili inafuatilia hali mpya na umaalumu mpya katika sekta hiyo.

    Sheria ya kulinda haki za watoto wadogo imehusisha haki za watoto na kanuni za kimsingi za kulinda watoto, na miswada ya marekebisho imeongeza kanuni nyingi mpya. Mkurugenzi wa Kamati ya ujenzi wa jamii kwenye Bunge la Umma la China Bw. He Yiting anasema:

    "Miswada ya marekebisho imeongeza kanuni zinazonufaisha zaidi watoto; kuimarisha jukumu la kwanza linalotakiwa kubebwa na wazazi au wasimamizi wengine; kuweka wazi kwamba endapo wasimamizi wa watoto hawawezi kutimiza majukumu yao ya usimamizi, serikali itachukua nafasi yao kutekeleza majukumu hayo; pia kuongeza mfumo wa utoaji wa ripoti baada ya haki za watoto kukiukwa."

    Takwimu zimeonesha kuwa, asilimia 6 ya watoto na vijana wana uraibu na mtandao wa Internet duniani, kiwango hicho kimefikia asilimia 10 nchini China. Kutokana na hali hii, mahitaji ya jamii za ngazi mbalimbali kuhusu kutunga sheria ya kuzuia watoto kutawaliwa na mtandao wa Internet yamekuwa yakiongezeka. Hivyo mswada wa marekebisho kuhusu sheria ya kulinda haki za watoto umeandaa sehemu kuhusu "hatua za kulinda watoto kwenye mtandao wa Internet". Bw. He Yiting anasema:

    "Ulinzi wa mtoto kwenye mtandao wa Internet unahusisha kanuni za ulinzi wa watoto kwenye mtandao wa Internet, usimamizi wa mazingira ya mtandao huo, majukumu ya kampuni zinazohusika, usimamizi wa habari kwenye mtandao wa Internet, ulinzi wa taarifa binafasi kwenye mtandao huo, na kuzuia watoto kutawaliwa na mtandao wa Internet."

    Aidha Mswada huo umeweka kanuni mpya ili kutatua tatizo kuhusu watoto wanaofanya makosa mabaya lakini wanaepuka adhabu kutokana na umri mdogo, lakini kutokana na ukosefu wa hatua za kurekebisha tabia yao, waliendelea na uhalifu baada ya kuwa watu wazima.

    Pia mswada huo umeimarisha majukumu yanayotakiwa kubebwa na familia, shule na mashirika ya serikali, ili kuzuia kadiri iwezekanavyo watoto kuwa wahalifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako