• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano kati ya China na Marekani hauwezi kuvunjwa

    (GMT+08:00) 2019-10-22 18:26:56

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, si kitendo cha kimantiki kuvunja uhusiano kati ya China na Marekani ambazo ni makundi makubwa ya kiuchumi duniani.

    Waziri msaidizi wa Marekani Bw. Chad Sbragia aliposhiriki kwenye Kongamano la Xiangshan la Beijing amesema, Marekani haitaki kuvunja uhusiano kati yake na China, wala haitaki nchi yoyote kuchagua upande wa kuunga mkono. Bali Marekani inafanya marekebisho na kutafuta uwiano kwenye uhusiano kati yake na China.

    Akizungumzai kauli hiyo, Bibi Hua amesema, kufungua mlango na ushirikiano ni njia sahihi, na China inazidi kupanua ufunguaji mlango kwa nchi zote duniani ikiwemo Marekani. Pia amesema China inataka Marekani ifungue mlango kwa China na kupunguza vikwazo visivyo mwafaka, hali inayoendana na maslahi ya pande zote mbili na matarajio ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako