• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa mkutano wa maendeleo ya nishati yenye uchafuzi mdogo mjini Taiyuan

    (GMT+08:00) 2019-10-22 19:09:03

    Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa mkutano wa maendeleo ya nishati yenye uchafuzi mdogo ulioanza leo mjini Taiyuan, mkoani Shanxi.

    Katika barua hiyo, Rais Xi amesema maendeleo ya nishati yenye uchafuzi mdogo wa hewa yanahusiana na mustakbali wa binadamu, na China inafuatilia maanani maendeleo ya nishati hiyo na kukuza kikamilifu matumizi ya nishati, ugavi, teknolojia na mageuzi ya kimuundo.

    Rais Xi ameongeza kuwa, China iko tayari kufanya kazi na jamii ya kimataifa ili kuimarisha ushirikiano wa nishati katika nyanja zote, kudumisha usalama wa nishati, kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa, kulinda mazingira ya kiikolojia, kudumisha maendeleo endelevu, na kuwanufaisha watu wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako