• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Uingereza lakataa ajenda ya utungaji wa sheria kuhusu Brexit

    (GMT+08:00) 2019-10-23 08:56:57

    Baraza la chini la bunge la Uingereza limepiga kura na kukataa ajenda ya utungaji wa sheria iliyotolewa na waziri mkuu Bw. Boris Johnson ili kuhimiza makubaliano ya Brexit yapitishwe haraka na bunge. Hii imeonesha kuwa uwezekano wa kuahirishwa kwa ajenda ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya unazidi kuongezeka.

    Bw. Johnson amesikitishwa na matokeo hayo, na kusema kupinga ajenda hiyo iliyotolewa na serikali ni kuunga mkono kuahirisha Brexit, na hii italeta sintofahamu nyingi kwa Uingereza. Amesema atasitisha ajenda ya utungaji wa sheria kuhusu kujitoa Umoja wa Ulaya, na kusubiri majibu ya Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako