• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Pep Guardiola amwagia sifa kedekede Raheem Sterling na kumuita mchezaji mwenye kipaji maalumu baada ya hat-trick

    (GMT+08:00) 2019-10-23 09:04:32

    Pep Guardiola amemwagia sifa kedekede Raheem Sterling na kumuita kama mtu mwenye kipaji maalumu baada ya jana kuingia nusu ya pili na kufunga hat-trick ndani ya dakika 11, ambapo ameisaidia Manchester City kuivuruga vibaya Atalanta kwa kuondoka na ushindi wa magoli 5-1 na kuimarisha mwanzo wao mzuri kwa 100% kwenye Ligi ya Mabingwa Kundi C. Sterling ni mfungaji anayeongoza wa Manchester City akiwa na magoli 12 aliyoyapata kwenye michezo 13 katika mashindano yote ya msimu huu na magoli aliyoyapata kwenye mchezo huu yamethibitisha uwezo wake mkubwa aliokuwa nao. Hata hivyo Guardiola anahisi Sterling ana uwezo mkubwa zaidi mbali na kufunga magoli tu. Amesema mwili wake uko imara, ana nguvu, na siku moja baada ya kucheza mechi anaweza kucheza mechi nyingine bila wasiwasi wowote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako