• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uwekezaji EPZ wafikia bil. 144/-

  (GMT+08:00) 2019-10-23 19:55:36
  Uwekezaji wa kampuni 11 zilizosajiliwa na Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA), kuwekeza katika viwanda vilivyoko kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (SEZ) wilayani Bagamoyo, umeongezeka na kufikia Dola milioni 62.84 ( takribani Sh. bilioni 144.53).

  Aidha, mapato ya fedha za kigeni yanayotarajiwa kupatikana kutokana na mauzo ya bidhaa za kampuni hizo nje ya nchi ni takribani Dola milioni 76.96 (karibu Sh. bilioni 177) wakati huohuo, zikizalishwa zaidi ya ajira 1,614.

  Mkurugenzi wa Uwezeshaji Uwekezaj wa EPZA, James Maziku, alisema haya mjini Kibaha, mkoani Pwani katika maonyesho ya viwanda na uwekezaji yanayoendelea mkoani hapa.

  Alisema uwekezaji na ujenzi wa viwanda vya kampuni mbili zilizosajiliwa katika maeneo maalumu ya uwekezaji wilayani Bagamoyo, umekamilika na kuanza kazi na nyingine zimefikia katika hatua mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako