• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: Nembo mpya ya Olimpiki 2024 ya Ufaransa yadhihakiwa

    (GMT+08:00) 2019-10-24 08:57:55

    Nembo mpya ya Olimpiki 2024 ambayo inapaswa kuonesha historia ya Ufaransa, sasa imekuwa gumzo na badala ya kusifiwa imekuwa ikidhihakiwa kwenye mitandao kutokana na kufanana sana na wanawake wa Paris. Nembo hiyo iliyozinduliwa Jumatatu, mtindo wake umeingizwa urembo wa sanaa ya wakati Paris ilipoandaa Michezo ya Olimpiki mwaka 1924, ikiwakilisha mwenge wa olimpiki ndani ya medali. Nembo hiyo pia imetiwa mdomo na sanamu ya Marianne, ambayo ni utambulisho wa uhuru na Jamhuri ya Ufaransa tangu mapinduzi ya mwaka 1789, urembo ambao baadhi ya watu wamekuwa wakiudhihaki kwa kuongezea vitu visivyo na ulazima. Wakazi wa Paris wameona kwa mara ya kwanza nembo hiyo mpya Jumatatu wakati ilipozinduliwa katika ukumbi maarufu wa sinema mjini Paris wa Grand Rex.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako