• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KASHFA: Mkuu wa Rusada asema Russia itarajie kupigwa marufuku kwenye michezo ya Olimpiki ya 2020

    (GMT+08:00) 2019-10-24 08:58:47

    Shirika la Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli la Russia (Rusada) limesema Russia lazima itarajie kupigwa marufuku kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 kwa kutuma data za maabara zisizoendana kwa wachunguzi. Shirika la Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli Duniani (Wada) mwezi uliopita limesema Russia inaweza kupigwa marufuku michezo yote mikubwa kutokana na kutoa data tofauti kwenye maabara ya Moscow. Jumatano, kamati ya Wada ilikutana na wataalamu walitathmini data na maelezo ya Russia kuhusu data hizo. Mkurugenzi wa Rusada Yuri Ganus amesema kikosi cha olimpiki cha Russia kitazuiwa kushiriki michezo yote ya Tokyo, na kwamba huenda hatua hiyo pia ikatekelezwa katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya hapa China mwaka 2022. Ganus anayedai kuwa Rusada haihusiki na kitendo chochote cha kubadilisha data kwasababu haikuwa na uwezo wa kufikia database, amesema anaamini maelezo yaliyowasilishwa na waziri wa michezo wa Russia Pavel Kolobkov hayatairidhisha Wada. Ganus pia anatarajia adhabu nyingine zikiwemo faini, kufungiwa kufanya mashindano ya kimataifa nchini Russia na nchi hiyo kuondolewa kwenye mashirikisho ya michezo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako