• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: La Liga yafikiria kuchukua hatua za kisheria kuhusu tarehe mpya ya mechi ya  El Clasico

    (GMT+08:00) 2019-10-24 08:59:30

    La Liga inafikiria kuchukua hatua za kisheria baada ya Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) kuahirisha mechi ya El Clasico kati ya Barcelona na Real Madrid na kupangiwa tarehe nyingine ambayo ni 18 Disemba. Awali mechi hiyo ilipangwa kufanyika Jumamosi huko Barcelona lakini imebadilishwa kwa ombi la La Liga kutokana na machafuko baada ya viongozi tisa wa wafarakanishani wa Catalonia kufungwa mapema mwezi huu. La Liga ilipendekea mechi hiyo iwe Disemba 4. Baada ya kuombwa kukubali tarehe mpya na kamati ya mashindano ya RFEF, ambao wamesaini umauzi huo Jumatano, timu zote mbili zikakubali Jumatano ya Disemba 18. Raundi ya kwanza ya michuano ya Copa del Rey itafanyika siku hiyohiyo. Awali Barcelona na Real Madrid hawakukubaliana na uamuzi wa La Liga wa kubadilisha mechi na kuchezwa Madrid.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako