• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Watanzania watumbukiwa nyongo baada ya goli la Samatta kukataliwa KRC Genk ilipovaana na Liverpool

    (GMT+08:00) 2019-10-24 08:59:57

    Usiku wa Octoba 23 ulikuwa usiku wa kihistoria kwa mtanzania Mbwana Samatta kwani alikuwa anacheza dhidi ya Liverpool huku akibeba unahodha wa KRC Genk katika mchezo huo wa UEFA Champions League. Hata hivyo kiu ya Watanzania wengi waliokuwa wanatamani kuona Mbwana Samatta akifunga goli dhidi ya Liverpool iliyokuwa chini ya safu ya ulinzi mkali wa Virgil van Dijk katika uwanja wa Luminus haikukatika baada ya mchezo huo kumalizika kwa Genk kupoteza 4-1 huku goli alilofunga mtanzania Mbwana Samatta likikataliwa na refa Slavko Vincic baada ya kuangalia VAR na kudai kuwa aliotea. Magoli ya Liverpool yalifungwa na Chamberlain dakika ya 2 na 57, Sadio Mane dakika ya 77 na Mo Salah dakika ya 86, huku la Genk likifungwa na Odey dakika ya 88, Samatta anaacha historia vichwani mwa watanzania kwa kuwa mtanzania wa kwanza kucheza dhidi ya Liverpool. Naye Lionel Messi Jumatano alivunja rikodi na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika misimu 15 mfululizo ya Champions League huku Barcelona ikiondoka na ushindi mwembamba wa 2-1 dhidi ya Slavia Prague.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako