• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Sintofahamu yaibuka siku chache kabla ya uchaguzi wa kiongozi wa Shirikisho la soka Kenya

    (GMT+08:00) 2019-10-24 17:28:35
    Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya Nick Mwendwa, ni mgombea pekee aliyewasilisha fomu zake kwa bodi inayoandaa uchaguzi wa kiongozi wa soka nchini humo. Wagombea wengine, wakiongozwa na rais wa zamani Sam Nyamweya, Moses Akaranga, Alex Ole Magelo na Steve Mburu hawakujitokeza kwa madai kuwa, bodi itakayosimamia uchaguzi huo, ilibadilisha sheria ili kumpendelea Mwendwa. Hata hivyo, Mwenyekiti wa bodi Edwin Wamukoya amesisitiza kuwa, siku ya Jumatano ilikuwa ya mwisho kwa waliokuwa na nia kurudisha fomu zao na sasa mlango umefungwa. Nyamweya amesema, malalamishi yao yako Mahakamani na kamati maalum inayoshughulikia masuala ya michezo nchini humo na anaamini kuwa madai yao yatashughulikiwa.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako