• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifurushi vya Safaricom vya data,sms,na kupiga simu sasa havina muda wa kuchina

    (GMT+08:00) 2019-10-24 19:44:01
    Kampuni ya Safaricom imetangaza kuanza uuzaji wa vifurushi vya intaneti, kupiga simu, na kutuma ujumbe mfupi,visivyo na muda wa ukomo.

    Hatua hii imejiri wakati kukiwa na kesi mahakamani ambapo wakili Adrian Kamotho aliishtaki kampuni hiyo pamoja na Airtel Kenya kwa kuweka muda wa vifurushi kupoteza thamani.

    Chini ya mpango huu mpya unaoanza kutekelezwa mara moja, zaidi ya wateja 33 milioni wa Safaricom wanayo fursa ya kununua vifurushi vya data na muda wa kupiga simu kuanzia kiwango chochote cha shilingi moja na kuendelea.

    Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom Michael Joseph,alisema kama pendekezo la kudumu, wateja wanaonunua mipango ya kupiga simu na kutuma SMS kwa kubonyeza *544# watapata asilimia 50 ya muda wa ziada kuongea kila wanapofanya hivyo ili wapate fursa ya kuongea zaidi kwa gharama nafuu.

    Wateja wengi wamefurahishwa na hatua hii ya kutokuwa na muda wa vifurushi vya intaneti,sms,na maongezi kupoteza thamani au kuwa na ukomo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako