• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hofu yatawala wakati IAAF ikipanga kuondoa baadhi ya fani kwenye mbio za Diamond

    (GMT+08:00) 2019-10-25 08:39:25

    Wanariadha wa Kenya huenda wakapoteza kiasi kikubwa cha posho kwenye mbio za Diamond League, iwapo Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), litatekeleza pendekezo la kushirikisha fani 12 pekee kwenye kivumbi hicho kuanzia msimu ujao. Mapema mwaka 2019 mataifa ya Kenya na Ethiopia ambayo ni ngome ya watimkaji mahiri katika mbio za masafa marefu yalipinga pendekezo la IAAF kuondoa fani za mbio za mita 5,000 na mita 10,000 kwenye mbio za Diamond League. Jumanne wiki hii, Kamati Kuu ya Diamond League ilitangaza kwamba huenda wasimamizi wa mbio hizo wakapunguza fani za msimu huu hadi 12 au 11 pekee kutokana na ufupi wa muda uliopo katika kalenda ya riadha za muhula ujao.

    Kulingana na IAAF, maamuzi ya mwisho kuhusu jinsi kivumbi cha Diamond League kitakavyoendeshwa mwakani yatatangazwa rasmi mapema mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako