• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yatishia Kenya kuipiga marufuku kushiriki mechi za kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-10-25 08:39:48

    Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), limeionya Kenya kuwa liko katika hatari ya kupigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote ya soka endapo mlalamishi atashinda kesi iliyowasilishwa dhidi ya Bodi ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Nchini (FKF). Kupita barua pepe iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa FKF, siku ya Jumatano, Oktoba 24 kutoka kwa kaimu Afisa Mkuu wa Uanachama Veron Mosengo, alisema kuwa mshtakiwa huenda akapigwa marufuku kushiriki michezo yote ya soka. Ujumbe huo ambao pia ulitumwa kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), uliikumbusha FKF kuwa ni makosa kwa ugomvi katika soka kuwasilishwa katika mahakama ya kawaida. Kesi hiyo iliwasilishwa katika Mahakama Kuu na George Mwaura, ambaye anataka idhini ya kusitishwa kwa uchaguzi unaotazamiwa kuandaliwa hivi karibuni hadi sheria ya bodi ya uchaguzi iliyobuniwa katika mkutano wa kila mwaka wa FKF kuzingatiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako