• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kilimanjaro Queens yapangwa kundi moja na ndugu zao Zanzibar kwenye CECAFA Challenge wanawake

    (GMT+08:00) 2019-10-25 08:40:10

    Wenyeji, Tanzania Bara wamepangwa Kundi A pamoja na ndugu zao, Zanzibar, Burundi na Sudan Kusini katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge wanawake) inayotarajiwa kuanza Novemba 14 hadi 24 mjini Dar es Salaam. Kundi B linaundwa na timu za Ethiopia, Kenya, Uganda na Djibouti huku Kilimanjaro Queens ambao pia ndio mabingwa watetezi watafungua dimba na Sudan Kusini Novemba 14, kabla ya kumenyana na Burundi Novemba 16 na kukamilisha mechi zao za Kundi A kwa kumenyana na Zanzibar Novemba 18. Challenge ya wanawake inafanyika kwa mara ya tatu katika historia mwaka huu baada ya 2016 Jinja nchini Uganda na 2018 mjini Kigali, Rwanda mara zote Kilimanjaro Queens wanabeba taji hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako