• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dereck Chisora aomba radhi kwa kusema atamuua mpinzani wake David Price

    (GMT+08:00) 2019-10-25 08:40:37

    Bondia wa Uingereza Dereck Chisora ameomba radhi kwa kusema atamuua mpinzani wake David Price. Kauli hiyo ameitoa siku tisa tu baada ya bondia wa Marekani Patrick Day kufariki akiwa na umri wa miaka 27 baada ya kusumbuliwa na majeraha ya ubongo aliyoyapata wakati anapambana. Akiongea kwenye mkutano na wanahabari kabla ya pambano la uzani wa juu litakalofanyika Jumamosi katika ulingo wa O2 Arena, Chisora, mwenye miaka 35, alisema na hapa nanukuu "Nitamuua huyu jamaa naapa kwa Mungu" Lakini baada ya hapo aliomba radhi kwa kusema hivyo na kusema hilo sio kusudi lake, ila limeponyoka tu kwani ulimi hauna mfupa. Day alipoteza fahamu baada ya kupigwa kwenye raundi ya 10 na Charles Conwell kwenye pambano la super welterweight Oktoba 12 huko Chicago, na kufariki baada ya siku nne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako