• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa kuanzisha mjadala wa kimataifa katika kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa mwakani

    (GMT+08:00) 2019-10-25 08:53:56

    Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwake yatakayofanyika mwaka ujao yatakuwa makubwa zaidi kufanyika duniani.

    Katika kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa, ambayo ilifanyika jana, Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres amesema, maadhimisho ya mwaka ujao yatakuwa na mijadala mikubwa ya kimataifa na jumuishi itakayohusu nafasi ya ushirikiano wa kimataifa katika kujenga siku za baadaye.

    Kuanzia Januari mwaka ujao, Umoja wa Mataifa utafanya mijadala duniani kwa lengo la kuwafikia watu wote duniani, kusikiliza matarajio na wasiwasi wao, na kujifunza kutokana na uzoefu wao.

    Siku ya Umoja wa mataifa inayoadhimishwa Oktoba 24 kila mwaka, inaashiria kumbukumbu ya kuanza kutekelezwa kwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa mwaka 1945.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako