• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa China wafanya mawasiliano ya karibu na Polisi wa Uingereza kuhusu ripoti za miili ya watu iliyokutwa kwenye kontena

    (GMT+08:00) 2019-10-25 08:54:18

    Ubalozi wa China nchini Uingereza umesema unawasiliana kwa karibu na Polisi nchini humo kutafuta ufafanuzi na uthibitisho kutokana na taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa miili ya watu 39 iliyokutwa kwenye lori moja huko Essex ni ya raia wa China.

    Taarifa iliyotolewa na Ubalozi huo imesema, wamesikitishwa na vifo vya watu hao, na wanawasiliana kwa karibu na polisi ili kupata ufafanuzi na uhakika wa habari hizo.

    Alhamis usiku, msemaji wa ubalozi huo alisema polisi wanatafuta kuwatambua watu waliofariki, ambao mpaka sasa utaifa wao hauwezi kuthibitishwa. Amesema ubalozi huo umewataka polisi na idara nyingine husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako