• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Misri na Ehiopia zakubaliana kurejesha mazungumzo kuhusu suala la bwawa la Nile

  (GMT+08:00) 2019-10-25 14:35:17

  Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misiri na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wamekubaliana kurejesha mara moja kazi ya kamati ya kiufundi ya bwawa la GERD.

  Taarifa iliyotolewa na msemaji wa ikulu ya Misri Bassam Rady inasema, kamati hiyo inalenga kufikia makubaliano ya mwisho ya kanuni ya kujaza na kuendesha bwawa hilo.

  Makubaliano hayo yamefikiwa katika mkutano kati ya viongozi hao wawili kando ya mkutano wa kilele kati ya Russia na Afrika unaofanyika Sochi, nchini Russia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako