• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa kuanzisha mazungumzo kuhusu mustakabali wa siku za baadaye za binadamu

    (GMT+08:00) 2019-10-25 18:32:26

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametangaza kuwa Umoja huo utaanzisha mazungumzo makubwa zaidi katika historia kuhusu mustakabali wa binadamu.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, kuanzia mwezi Januari mwaka 2020 Umoja wa Mataifa utaanzisha mazungumzo ya kuvuka mipaka, idara katika sehemu mbalimbali duniani, ambao utasikiliza kwa pande zote ufuatiliaji, wasiwasi na matumaini ya watu kote duniani kuhusu utatuzi wa masuala ya dunia nzima.

    Bw. Guterres amesema mazungumzo hayo yatahusisha kwa kiasi kikubwa zaidi watu wa nchi mbalimbali duniani, huku yakizingatia kusikiliza sauti za vijana na kundi la watu wenye hali duni katika mambo ya kimataifa.

    Mbali na hayo Bw. Guterres leo pia ametoa ripoti ikihimiza nchi mbalimbali kuongeza idadi ya wabunge na mawaziri wanawake.

    Ripoti hiyo inayoitwa "Wanawake na Amani na Usalama" imesema, hivi sasa kiwango cha wabunge wanawake ni asilimia 24.3 tu kote duniani, hata baadhi ya nchi hazina wabunge au mawaziri wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako