• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 30 wauawa na wengine zaidi ya 2,300 kujeruhiwa kwenye maandamano nchini Iraq

    (GMT+08:00) 2019-10-26 18:18:23

    Takriban watu 30 wameuawa na wengine zaidi ya 2,300 kujeruhiwa huku maelfu ya Wairaq wenye hasira wakikusanyika Ijumaa kwenye miji kadhaa ya Iraq ukiwemo mji mkuu Baghdad, katika wimbi jipya la maandamano ya kuipinga serikali kutokana na hali mbaya ya maisha. Tangu jana asubuhi waandamanaji wamevamia uwanja wa Tahrir upande wa mashariki ya Mto Tigris na mara kwa mara kutaka kuvuka daraja lililo karibu la Jumhouriyah ili kufika eneo la utawala wa serikali lakini walikuwa wakizuiwa na polisi. Maandamo pia yalizuka jana kwenye miji mingine mingi ikiwemo ya majimbo kadhaa ya kusini na kati ambako waandamanaji wanataka kufanyika mageuzi, kuwajibishwa mafisadi na fursa za ajira.

    Shehe wa dhehebu la Shia Ayatollah Ali al-Sistani amewataka waandamanaji na vikosi vya usalama kujitolea kikamilifu kuleta amani na kuzuia vurugu na uharibifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako