• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vurugu mpya nchini Nigeria zawalazimisha zaidi ya watu laki 1.4 kukimbia makazi yao mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-10-26 18:18:46

    Vurugu mpya ambazo nyingi zinasababishwa na kundi la Boko Haram kaskzini mashariki mwa Nigeria, zimewalazimisha zaidi ya watu laki 1.4 kukimbia makazi yao mwaka huu.

    Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Amefafanua kuwa wakulima wengi wamekosa misimu mingi ya upandaji na zaidi ya watu miloni 3 wanakosa chakula. Amesema Umoja wa Mataifa na washirika wake wamekuwa wakitoa misaada ya kibidamu kaskzini mashariki mwa Nigeria tangu kuanza kwa vurugu hizo, na kwamba mwaka 2019 pekee, hadi sasa wametoa msaada mkubwa wa kuokoa maisha kwa zaidi ya watu milioni 3.8.

    Hata hivyo Dujarric amesema zaidi ya watu milioni 7 kwa sasa wanahitaji msaada wa kibinadamu katika majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako