• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Njia ya maendeleo na mafanikio ya haki za binadamu nchini China yapongezwa na Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2019-10-27 18:18:55

    Njia ya maendeleo na mafanikio kwenye maswala ya haki za binadamu nchini China imepongezwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya maendeleo ulioandaliwa na ujumbe wa kudumu wa China katika umoja huo.

    Naibu mkurugenzi wa kanda ya Latin Amerika na Caribbean wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Bw. Lenni Montiel, amesema China ni mfano wa kuigwa kwa nchi yoyote inayoendelea duniani, kuhusu vipi nchini inaweza kujiendeleza kwa kutekeleza mipango yake ya maendeleo.

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuweka umuhimu mkubwa kwenye hali ya maendeleo, na kuweka maendeleo kuwa kiini cha mipango ya sera na kuhimiza utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako