• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la serikali ya Libya inayoungwa mkono na UM lakamata askari 8 wa jeshi la mashariki mwa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-10-28 08:49:54

    Jeshi la serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa limetangaza kuwakamata askari nane wa jeshi la mashariki mwa nchi hiyo kwenye eneo la kusini mwa Tripoli.

    Msemaji wa jeshi hilo amesema askari hao walikamatwa kwenye eneo la Ain Zara walipojaribu kujipenyeza kwenye eneo hilo. Amesema jeshi hilo limetwaa udhibiti wa eneo kubwa kusini mwa Tripoli, na kuteketeza magari mawili wa jeshi la upinzani lenye makao makuu mashariki mwa nchi hiyo.

    Jeshi la Libya mashariki mwa nchi limeanzisha kampeni ya kijeshi tangu mapema mwezi Aprili mjini Tripoli na katika maeneo ya karibu, likijaribu kuutwaa mji huo na kupindua serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako