• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Alphonce Simbu aitoa kimasomaso Tanzania kwa kuondoka na fedha kwenye michezo ya majeshi duniani ya China

    (GMT+08:00) 2019-10-28 08:56:22

    Mwanariadha Alphonce Simbu amefanikiwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano ya majeshi ya Dunia yaliyomalizika jana hapa nchini China, na kuitoa kimasomaso nchi hiyo kwa kujinyakulia medali ya Fedha. Mwanariadha huyo akiwakilisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, alimaliza baada kukimbia kwa saa 2:11:16 huku akiwaahinda wakimbiaji wengine 95 kutoka nchi zaidi ya 30. Katika mbio hizo mshindi wa kwanza aliyejizolea medali ya dhahabu ni Luche Sumi kutoja Bahrain aliyekimbia kwa saa 2:08:28, na mshindi wa tatu aliyeondoka na shaba ni mwanariadha kutoka Rwanda John Hakizimana akiyekimbia kwa karibu nyuma ya Simbu kwa saa 2:11:19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako