• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Afrika Kusini yaibanjua Wales kwa 19-16 na kufika fainali ya Kombe la Dunia la Raga

    (GMT+08:00) 2019-10-28 08:57:09

    Afrika Kusini jana ilijikatia tiketi ya kucheza fainali ya Kombe la Dunia la Raga huko Yokohama Japani, baada ya Handre Pollard kufunga pointi 14 na kuiondoa kifua mbele timu ya Rassie Erasmus kwenye mpambano mkali ulioshia kwa Afrika Kusini kushinda 19-16 dhidi ya Wales. Pollard alipiga penalti zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika huku kizaazaa kizuka kwa mechi kuongezwa muda wa ziada baada ya matokeo kuwa sare ya 16-16. Mpambano huo uliokuwa wa kukata na shoka umeshuhudia mabingwa hao wa kombe la Dunia mwaka 1995 na 2007 kuwabwaga Wales katika shindano lao la tatu la nusu fainali baada ya huko nyuma kupoteza katika mwaka 2011 na 1987. Afrika Kusini sasa itavaana na England katika hatua ya fainali siku ya Jumamosi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako