• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Yanga FC yachungulia mlango wa kutokea Afrika, yachapwa 2-1 na Pyramids FC Mwanza

    (GMT+08:00) 2019-10-28 08:57:40

    Klabu ya Yanga ya Tanzania imejiweka kwenye mazingira magumu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania nafasi hiyo jioni ya jana Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa wana kazi ya kupindua meza mbele ya wapinzani wao Pyramids FC nchini Misri kwenye mchezo wa marudio utakaopigwa baada ya wiki mbili. Mchezo wa jana Oktoba 27 ulioanza kwa kasi, Yanga ilikubali kwenda mapumziko ikiwa imefungwa bao 1-0. Kipindi cha pili walianza kwa kasi bado mambo yalikuwa magumu kwa Yanga na kuwapa nafasi wapinzani wao kuandika bao la pili. Iliwachukua Yanga dakika 90 kuandika bao la kwanza kupitia kwa Papy Tshishimbi kwa shuti kali akimalizia pasi ya Kaseke. Ili kusonga mbele Yanga itatakiwa kushinda mabao 2 ugenini na wanatakiwa kulinda lango lao lisitikiswe na wapinzani. Yanga itamkosa beki kisiki, Kelvin Yondan ambaye ameonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na kadi mbili za njano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako