• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iraq ilitoa taarifa muhimu za kijasusi kwa ajili ya operesheni ya jeshi la Marekani dhidi ya al-Baghdadi

    (GMT+08:00) 2019-10-28 09:06:40

    Kamandi ya operesheni ya pamoja nchini Iraq imetoa taarifa ikisema, baada ya kumtafuta Abu Bakr al-Baghdadi kwa muda wa mwaka mmoja, idara ya ujasusi ya Iraq ilithibitisha mahali alipojificha kiongozi huyo wa kundi la IS nchini Syria, na kutoa taarifa muhimu za kijasusi kwa operesheni ya jeshi la Marekani dhidi yake.

    Taarifa imesema idara ya upelelezi ya Iraq iliunda kikosi kazi maalumu baada ya kumtafuta al-Baghdadi kwa muda wa mwaka mmoja, kikosi kazi hicho kilipata habari sahihi na kuthibitisha mahali katika jimbo la Idlib nchini Syria ambapo al-Baghdadi na wenzake walikuwa wanajificha. Jeshi la Marekani lilishirikiana na idara ya ujasusi ya Iraq, walifanya operesheni ya kijeshi usiku wa tarehe 26, na kuwaangamiza al-Baghdadi na wenzake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako