• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Syria yafurahia kuondoka kwa Kundi la Wakurdi kaskazini mwa Syria

    (GMT+08:00) 2019-10-28 09:12:09

    Wizara ya mambo ya nje ya Syria imetoa taarifa ikisema inafurahia Kundi la Wakurdi kuondoka kaskazini mwa Syria.

    Shirika la habari la Syria limenukuu taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo ikisema Kundi la Wakurdi limeanza kuondoka kutoka eneo la kilomita 30 kusini mwa mpaka kati ya Syria na Uturuki, kitendo ambacho kilianza baada ya "uratibu wa moja kwa moja" na jeshi la Syria. Taarifa hiyo imesema kuondoka kwa Kundi la Wakurdi kumeifanya Uturuki ipoteze kisingizio cha kuivamia Syria.

    Taarifa hiyo imeongeza kuwa serikali ya Syria italinda muundo wa makabila anuwai, na kuwafungulia mlango raia wanaorejea tena katika jamii ya Syria, na kuwa na mshikamano wa kikabila.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako