• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wakubali kuongeza muda wa Brexit hadi Januari 31 mwaka ujao

    (GMT+08:00) 2019-10-28 19:23:58

    Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk amesema nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubali kuwa watapokea ombi la Uingereza kuongeza muda wa Brexit mpaka Januari 31 mwaka ujao.

    Akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Bw. Tusk amesema uamuzi huo unatarajiwa kuwa rasmi kimaandishi.

    Tarehe 20 mwezi huu, waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson alipeleka barua kwa Tusk akiomba kuongezewa muda zaidi wa kifungu cha 50, akitaka muda wa Brexit kuongezwa hadi Januari 31, mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako