• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China ahimiza umuhimu wa suluhisho la nchi mbili kutatua mgogoro wa Palestina

    (GMT+08:00) 2019-10-29 08:39:09

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa mataifa Balozi Zhang Jun amesema lengo la jumla la suluhisho la nchi mbili linatakiwa kufuatwa kwenye utatuzi wa mgogoro wa Palestina.

    Akiongea kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Balozi Zhang amesema, kanuni ya utatuzi wa nchi mbili, na "ardhi kwa amani" ni msingi wa sheria za kimataifa. Amesema kuwa na nchi huru ni haki ya kimsingi ya watu wa Palestina, na jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufuata suluhisho la nchi mbili, maazimio husika ya Umoja wa mataifa, kanuni ya ardhi kwa amani na makubaliano mengine, ili kurudisha mchakato wa amani ya mashariki ya kati.

    Pia ameitaka Israel kukomesha ujenzi wa makazi kwenye maeneo ya Palestina, na kutumia mabavu dhidi ya raia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako