• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa wataja majanga ya asili na mahitaji ya misaada ya kibinadamu barani Afrika

  (GMT+08:00) 2019-10-29 08:39:31

  Umoja wa mataifa umetaja majanga ya asili yanayohusiana na hali ya hewa katika nchi kadhaa za Afrika, ikiwa ni pamoja na mafuriko nchini Somalia na Sudan Kusini, na ukame nchini Zambia.

  Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema mvua za msimu tayari zimeanza nchini Somalia na kusababisha mafuriko katika majimbo ya Hirshabelle, Jubaland na Kusini Magharibi. Amesema watu laki 1.8 wamehama makazi yao, mashamba, miundo mbinu na barabara vimeharibiwa, na katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa vibaya shughuli za maisha zimekwama.

  Nchini Sudan Kusini watu laki 9 ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa ndani ya jamii zinazowahifadhi wameathiriwa, na mvua ambazo zinatarajiwa kuendelea kunyesha kwa wiki nne hadi sita zijazo. Mvua hizo zimeyakumba maeneo ambayo tayari yalikuwa yanakabiliwa na msukosuko wa kibinadamu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako