• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Walinda amani wa China wamsafirisha polisi wa Misri aliyejeruhiwa vibaya nchini Sudan kwa ajili ya matibabu

  (GMT+08:00) 2019-10-29 08:44:24

  Walinda amani kutoka China wamefanikiwa kumsafirisha mlinzi wa amani kutoka Misri aliyejeruhiwa vibaya nchini Sudan kwa ajili ya matibabu.

  Kikosi cha tatu cha helikopta cha China (CMUHU03) kimesema helikopta moja wa kikosi hicho kinachotekeleza majukumu kwenye eneo la Darfur nchini Sudan ilimsafirisha kwa dharura mlinda amani kutoka Misri aliyezirai baada ya kujeruhiwa kichwani, kutoka Shagil Tbaya hadi El Fasher Jumapili iliyopita. Baada ya kufikishwa El Fasher ndani ya saa mbili, ofisa huyo alipelekwa Khartoum kwa ajili ya matibabu zaidi kwa ndege nyingine ya Umoja wa Mataifa.

  Kikosi cha Polisi wa kulinda amani cha Misri kimewashukuru wenzao wa China kwa msaada wao wa haraka, ambao umesaidia kuokoa maisha ya majeruhi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako