• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza maendeleo ya mapambano dhidi ya IS

    (GMT+08:00) 2019-10-29 08:58:47

    Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema katibu mkuu wa umoja huo Bw. Antonio Guterres amepongeza maendeleo ya mapambano dhidi ya kundi la IS kutokana na kifo cha kiongozi wa kundi hilo Abu Bakr al-Baghdadi.

    Bw. Haq amesema, kundi la IS limefanya uhalifu mkubwa na kuleta janga na vifo kwa maelfu ya wanaume, wanawake na watoto. Ameongeza kuwa maendeleo yoyote ya mapambano dhidi ya kundi IS yanakaribishwa.

    Bw. Haq amesema Umoja wa Mataifa na mashirika yake umewataka nchi wanachama wake zishirikiane na kupambana kwa pamoja na kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako