• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya magharibi vyaaibika kwa kubagua China

    (GMT+08:00) 2019-10-29 16:07:30

    Waasia 39 waliogunduliwa kufariki kwenye lori la baridi ya nyuzi 25 chini ya sifuri, ni moja ya habari inayofuatiliwa zaidi na watu duniani. Wakati uraia wa watu hao bado haujatambuliwa, vyombo vya habari vya magharibi vimedai kuwa watu hao walitoka China.

    Kabla ya kupata ushahidi halisi wa kuthibitisha uraia wa wahamiaji haramu ambao miili yao ilikutwa kwenye lori nchini Uingereza, vyombo vya habari vya magharibi vilidai kuwa wanatoka China. Mtangazaji wa Shirika la Habari la Marekani CNN alimuuliza msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying kuwa, wakati China inapoadhimisha miaka 70 tangu kuasisiwa kwake, kwa nini Wachina hao wamekimbilia nchi za magharibi kwa njia haramu? Akimaanisha kuwa, China ina taabu kubwa katika mifumo yake ya kisiasa na kijamii, na mafanikio yaliyopatikana nchini humo hayawanufaishi wananchi wake, hivyo wachina wanataka kukimbilia nchi nyingine.

    Akijibu swali hilo linalotaka kuiabisha China, Bi. Hua Chunying amesema, jambo linalofaa zaidi kufanywa kwa wakati huu ni kuwaomboleza marehemu hao, na kuhusisha janga hili na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa China mpya kumeonesha ubaguzi wa vyombo vya habari vya magharibi kuhusu China.

    Habari mpya zinasema, huenda wahamiaji hao haramu walitokea Vietnam, kwani familia 24 za nchini humo zimetoa ripoti kwa polisi kwamba hawajui ndugu zao walipo huko Ulaya, naye balozi wa Vietnam nchini Uingereza amefika mahali janga hilo lilipotokea ili kulielewa zaidi.

    Baada ya kusikia janga hilo, tofauti na vyombo vya habari vya nchi za magharibi, wachina wengi hawakuamini kuwa wahamiaji hao walitoka China, kwani hivi sasa ni rahisi kwa wachina kupata visa ya kutalii nchini Uingereza, na hawana haja ya kuchagua njia ya hatari. Takwimu zilizotolewa na Kituo cha Utafiti wa Sayansi cha Ufaransa zinaonesha kuwa, ikilinganishwa na miaka ya 1990-2000, wahamiaji haramu wa kiuchumi kutoka China kwenye nchi za Ulaya wamepungua kwa kiasi kikubwa.

    Kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi, Wachina wana maisha bora. Hata hivyo si rahisi kusema hakuna Mchina anayetaka kuhamia nchi nyingine, lakini kwa bahati mbaya, mambo haya huhusishwa na mifumo ya kisiasa ya China. Kufuatia mawazo ya vyombo vya habari vya magharibi, China ina makosa ya kiasili, kwani inatekeleza mifumo tofauti ya kisiasa na kijamii na nchi za magharibi.

    Mtu akivaa miwaani yenye rangi moja kwa muda mrefu, ataona hakuna rangi nyingine duniani. Vyombo vya habari vya magharibi vinapaswa kuacha kubagua China, ili visijiaibishe vyenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako