• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la waziri mkuu wa Uingereza la kufanya uchaguzi mkuu mapema lakataliwa na bunge

    (GMT+08:00) 2019-10-29 18:53:28

    Pendekezo la waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson la kufanya uchaguzi mkuu mapema, limekataliwa na baraza la chini la bunge la nchi hiyo.

    Matokeo ya kura zilizopigwa jana katika baraza hilo yameonyesha kuwa, kura 299 ziliunga mkono pendekezo hilo na kura 70 zililipinga, lakini, kwa mujibu wa sheria, inapaswa kuungwa mkono na kura 434 ili kupitishwa. Wabunge wengi wa chama cha upinzaji waliacha kupiga kura.

    Hii ni mara ya tatu ya Bw. Johnson kuagiza kupiga kura kuhusu kufanya uchaguzi mkuu mapema, na anatarajia chama chake kitawala kitapata viti vyingi zaidi katika baraza la chini ili kupitisha makubaliano ya Brexit.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako